Jumatatu , 26th Mei , 2014

Rapa Kaligraph kutoka Kenya, ameendelea kusukuma mbele gemu yake ya muziki kwa kushirikiana kufanya kazi na msanii wa kimataifa, D Soul kutoka UK.

Kaligrap

Kazi hii inayokwenda kwa jina What You Need, inasimama kama kolabo ya kwanza kubwa kwa upande wa kimataifa kwa rapa huyu ambaye ameahidi kuwa muziki wake kuanzia sasa utakua ukitoka kwa ladha tofauti ambayo wengi hawajaizoea.

Kaligraph amesema kuwa, yeye sio muongeaji sana kwa kile anachokifanya sasa katika muziki, bali kazi zake ndio zitakazokuwa zinaongea na kuthibitisha uwezo wake.