"Kajala ni mama yangu sio wa Tanzania nzima" Paula

Ijumaa , 16th Jul , 2021

Mtoto wa staa wa filamu Kajala Masanja Paulah Kajala amewatolea uvivu wanaomshambulia mama yake kwenye mitandao ya kijamii kuhusu malezi anayopewa kwa kusema haiwahusu kwani Kajala ni mama yake yeye na sio mama wa Tanzania nzima.

Picha ya Kajala akiwa na mwanaye Paula

Akitoa dukuduku lake hilo kwenye insta story yake ya mtandao wa Instagram Paulah Kajala ameandika kuwa 

"Naombeni tuelewane Kajala ni mama yangu mimi na sio mama wa Tanzania nzima, awe mama mzuri au mama mbaya haiwahusu fuateni maisha yenu na mumuache peke yake".

Siku ya jana ilikuwa ni birthday party ya Paulah Kajala ambapo alionekana akijiachia zaidi na msanii Rayvanny mbele ya mama yake mzazi hali ambayo imefanya watu kujudge zaidi tukio hilo.