Jumatano , 3rd Jun , 2015

Staa wa Filamu Kajala Masanja, katika harakati za kupanua zaidi soko la usambazaji filamu hapa Tanzania, amesema kuwa filamu yake inayoitwa 'Pishu' imefanyika na kusambazwa chini ya usimamizi wake mwenyewe imefikia hatua nzuri inayompa moyo.

Staa wa filamu nchini Kajala Masanja

Kajala ambaye ameonesha mfano kwa wasanii wenzake kuwa inawezekana kuwafikia mashabiki kwa kazi endapo mtu atafanya kazi ya ziada kujisimamia mpaka mwisho, kwa kushirikiana na timu yake amesema kuwa kwa sapoti ya mashabiki anaamini amepiga hatua kubwa na anaweza kufika alipokuwa amepanga.