
Msanii Jux
Jux ambaye jana ameachia video ya ngoma yake mpya aliyomshirikisha Vannesa 'Sumaku', ametupia picha mitandaoni akionekana yupo Vacation kwenye Mbuga ya Serengeti akiwa na mwanadada mwingine.
Jux ameweka picha tofauti tofauti kwenye Instagram, huku zikiambatana na ujumbe kuwa ni 'Vocation' kwa maana ya mapumziko.
Licha ya Vanessa kuthibitisha kuwa wameachana na kilichobaki ni ushkaji tu, lakini bado maswali yalikuwa mengi lakini hili la Jux kuonekana na mwanadada mwenye asili ya kizungu, huenda likatoa majibu kuwa wawili hao wameachana.