Jumatano , 26th Feb , 2014

Kikaangoni Live ya ukurasa wa Facebook EATV leo imewakutanisha wapenda burudani na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Jux Vuitton kama anavyopenda mwenyewe kujiita, ambapo naye amepata nafasi ya kuchat na mashabiki wa kazi zake live kwa muda wa saa mbili mfululizo.

Jux katika zoezi hili ameweza kuweka mambo mengi wazi kumhusu yeye na kuwapatia mashabiki wake nafasi ya umfahamu zaidi pamoja na kufahamu kazi zake kwa undani.

Msanii huyu baada ya zoezi akapiga story na eNewz na akafunguka kuhusu Kikaango cha leo ambapo amesema amefurahuishwa kupata nafasi hii ya kujibu maswali ya mashabiki wake na pia kufahamu juu ya wanavyomchukulia, huku akisema swali kubwa lililokuwa likitaka ufafanuzi ni kuhusiana na yeye kufanya biashara ya dawa za kulevya, kitu ambacho amesema hakina ukweli wowote.

Baada ya Jux, kaa tayari kwa staa mwingine mkali zaidi juma lijalo tena katika Kikaangoni Live, ambayo inakujia kupitia www.facebook.com/eatv.tv pekee.