Ijumaa , 7th Nov , 2014

Siku ya leo marapa wakali kabisa hapa Bongo, One The Incediblke, Songa, Nikki Mbishi na mwanadada Lady Jay Dee wataongeza nakshi kwa TV yako kwa kuzindua video yao mpya ya 'Kupanda na Kushuka' kupita hapa EATV.

wasanii wa bongofleva One The Incredible, Jide na Nikki Mbishi

Kazi hii kali itatambulishwa rasmi na mastaa hawa katika kipindi cha FNL leo hii kuanzia saa nne usiku ambapo utapata nafasi maalum ya kuitazama yote kwa mara ya kwanza.

Video hii ambayo ni project ya kwanza kubwa kabisa kwa wasanii hawa ikiwa na muonekano na ladha tofauti kabisa, ni kazi ya muongozaji video mahiri, Adam Juma.