Picha ya Jay Z usiku wa tuzo za Grammy
Jay Z amefunguka hilo wakati anapokea tuzo ya ‘Dr Dre Global Impact Award’ akihoji kuwa Beyonce ana tuzo nyingi za Grammy kuliko mtu yeyote na nyimbo zake kutoka kwenye Album ndio zinachukua tuzo kwa nini hapewi tuzo ya Album bora ya mwaka.
“Inakuaje ana tuzo nyingi za Grammy kuliko mtu yeyote, halafu unakosa tuzo ya Album bora ya mwaka? Hiyo haifanyi kazi fikirieni kuhusu hilo, wengi wataenda nyumbani kuhisi kama ameibiwa” amesema Jay Z