Alhamisi , 16th Apr , 2015

Katika moja ya matukio makubwa kabisa katika muziki wake, Staa wa muziki Jaguar kutoka nchini Kenya anatarajiwa kutua nchini Marekani, kwaajili ya maonesho mawili makubwa mwishoni mwa wiki hii Atlanta na Massachusetts.

msanii wa nchini Kenya Jaguar

Onesho hilo la Jaguar linakuja baada ya kipindi kirefu cha kukosa burudani kutoka kwa msanii wa eneo hili la Afrika Mashariki, na hii ni kwa mujibu ya moja ya waratibu wa onesho hilo, Mary Bowers.

Staa huyo kwa sasa anafanya vizuri kupitia ngoma yake inayokwenda kwa jina la 'Huu Mwaka', ambayo nayo pia inaendelea kufanya vizuri kwenye chati mbalimbali katika vituo vya kimataifa na mtandaoni.