Jumamosi , 24th Oct , 2015

Rapa Izzo Business ameweka wazi kuwa kwa nafasi yake, anasaidia kunyanyua vipaji vya wasanii wana

Izzo Business

Rapa Izzo Business ameweka wazi kuwa kwa nafasi yake, anasaidia kunyanyua vipaji vya wasanii wanaochipukia kwa kutenga muda wake kutoa ushauri kama ambavyo binafsi ameweza kufanikiwa kwa kuzingatia mawazo na kujifunza kutoka kwa wasanii waliomtangulia.

Izzo B ameeleza kuwa, kwa wasanii wenye malengo ya kukua na vipaji ndani yao, huwa anachukua nafasi ya kuwajenga wawe wasanii bora wa baadaye, ushauri wake wa wazi kwao pembeni ya muziki ukiwa ni displine, heshima kwa kila mtu na kuzingatia muda.

Kwa maneno yake binafsi, mkali huyu anayeiwakilisha Mbeya anaweka bayana busara zake hapa.