Jumatatu , 16th Feb , 2015

Rapa Izzo Business, ambaye anajiweka sawa kwa ajili ya kudondosha projekti yake ya kwanza kabisa kwa mwaka 2015, amesema kuwa kazi hii inayokwenda kwa jina Kidawa itagusa na pia kubadili mahusiano mengi ya kimapenzi.

Izzo Business

Izzo amesema pia kuwa rekodi hii inakuwa ni ya kwanza kwake kusimamiwa kiitikio chake kizima na nyota wa kike ambaye ni Shaa, akiwataka mashabiki kukaa tayari kwa video makini kabisa ya kazi hiyo.