Jumanne , 8th Jul , 2014

Msanii wa miondoko ya Bongofleva nchini Tanzania Izzo Bisnezz hivi sasa ameamua kuupa muziki wa mapenzi kisogo na kuungana na nyimbo za kuwalenga watu ambao ni wa hali ya chini kwa kutoa traki mpya aliyoibatiza jina 'Walala hoi'.

Msanii wa bongo Izzo Bizness

Izzo Bisnezz ameongea na eNewz kuhusu yeye kuhamasika kutunga wimbo huo mpya ambao unatarajiwa kuachiwa rasmi kesho kupitia vyombo vya habari mbalimbali nchini.