
Irene Uwoya na Steve Nyerere
Akizungumza leo Julai 17, Mngereza amesema kufuatia wito huo, wao kama Baraza hawajapanga kuwachukulia hatua zozote zile za kisheria.
''Wajibu wa baraza ni kukaa na wasanii, halafu kuzungumza nao, na baraza linafanya kazi kwa mujibu wa sheria lililoziweka na kama uliona yale ni masuala ya fedha", amesema Mngereza.
Aidha kwa upande wake Steve Nyerere amekiri kupokea taarifa hizo na kwamba yeye kama msanii na BASATA ni Serikali, hivyo atafika kama alivyotakiwa.
Aidha Steve alipoulizwa kuhusu kitendo cha Irene Uwoya kuwatupia waandishi wa habari pesa, amejibu ''No Comment"