Jumatano , 25th Mar , 2015

Akiwa kama msanii wa muziki mkongwe aliyepitia uzoefu mbalimbali kiuchumi na kisanaa, staa wa muziki Inspekta Haroun amewashauri wasanii hususan wale wanaochipukia kutumia vizuri pesa zao na vilevile kuwekeza katika miradi tofauti nje ya muziki.

Msanii wa bongofleva nchini Inspecta Haroun

Inspekta a.k.a Babu amesema kuwa, kama msanii ni vizuri zaidi kuwa mjasiriamali pia kutokana na kuongeza kipato na kuwa na vyanzo vingi vya mapato ikiwa ni njia ya kuwaepusha na msongo wa mawazo.