Ijumaa , 13th Nov , 2015

Rapa Mkongwe katika gemu ya rap Bongo, Inspekta Haroun ametoa nasaha zake kwa wasanii wanaofanya muziki kwa sasa kuzingatia utajiri wa ladha mbalimbali za muziki ambazo wanaweza kujivunia hapa nchini.

Rapa Mkongwe katika gemu ya rap Bongo, Inspekta Haroun

Inspecta amesema ladha hizo ni kutoka makabila mengi na tofauti ya hapa nyumbani katika kujaribu kutengeneza ladha ambazo chanzo chake kitakuwa ni hapa.

Katika kufafanua hili, Inspekta mbali na sanaa anayofanya ameeleza kuwa binafsi ni mpenzi mkubwa wa Bendi kongwe ya Njenje kutokana na kuvutiwa na asili ya vionjo vyao, hii ikiwa ni kati ya siri kubwa za kudumu kwa kazi zao, kama anavyoeleza hapa.