Jumatatu , 5th Oct , 2015

Msanii madee ambae anafanya poa katika anga za Bongo Fleva, amesema idea ya wimbo wa Vuvula waliipata kutoka kwa Wazimbabwe ambao walikuwa wana ishi nao jirani walipoenda mapumzikoni nchini South Africa.

Madee ameyasema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na east Africa Radio, na kueleza hayo huku akifafanua maana ya neno la vuvula kuwa ni mtu mshamba

"Idea ya vuvula ilikuja wakati tuko zetu S.A tumeenda kupumzika kule, so tukawa tunakaa karibu na Wazim yani Wazimbabwe kwenye apartment moja, wao wakawa kila wakikaa wanaliongelea sana hilo neno Vuvula, ikabidi siku moja tuwaulize, wakasema vuvula ni mtu mshamba, mtu ambaye anafanya vitu ambaye haviko sawa kwenye jamii lakini ye anaviona viko sawa, kwa hiyo huyo ni vuvula", alisema Madee.

Pia Madee aliendelea kwa kusema kwamba baada ya hapo akaona ni neno zuri lenye asili ya kiafrika, na kuanza kuifanyia kazi nyimbo ya vuvula, na kuamua kumshirikisha Chege, kwani ndiye aliyekuwa analitaja sana neno hilo na alikuwa yuko karibu nae.

"Tukaona ni neno fulani hivi zuri na lina sound vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva pamoja na Afrika nzima kwa sababu ni neno ambalo limekaa Kiafrika, tukaenda studio tukakutana na beat kwa Mapoliso basi tukawa tunajiimbia tu Vuvula, nikaona kama inasound vizuri alafu Chege ndo alikuwa anaimba imba sana, kwa hiyo kwa sababu na mimi niko karibu sana na Chege, management zetu zinafanya kazi pamoja, sikuona tatizo kumshirikisha Chege", alisema Madee.