Alhamisi , 6th Jan , 2022

Kutoka 254 Kenya mrembo na mfanyabiashara Vera Sidika ameweka wazi idadi ya watoto anaotaka kuwa nao kwenye maisha yake ambao ni watoto watatu au wanne.

Picha ya Vera Sidika, Brown Mauzo na mtoto wao

Vera Sidika ameshea hilo kwenye Insta Story yake baada ya shabiki kumuuliza amepanga kupata watoto wangapi.

Pia ameeleza kwamba huenda mwishoni mwa mwaka huu 2022 akaongeza mtoto wa pili, kwa sasa ana mtoto mmoja wa kike aitwaye Asia Brown aliyempata na mpenzi wake Brown Mauzo.