Jumatano , 11th Mei , 2022

Baada ya picha za mtoto na mwanamke anayedai amezaa na Ibraah kusambaa mtandaoni, Harmonize amemtaka Ibrah amuone mtoto huyo ikiwezekana akafanye na vipimo.

Katikati picha ya mwanamke na mtoto anayesemekana ni wa Ibraah.

Harmonize kupitia insta story ameweka picha ya mwanamke na mtoto na kuandika

"Brother tulete huyu mfalme tutakopa, tutaiba ili mradi mkono uende kinywani, Nenda tu ukajiridhishe na DNA upate amani ya moyo ila huyu Chinga.."

Wiki kadhaa nyuma Ibraah kupitia instagram aliandika kwamba yeye hana mtoto baada ya kuibuka kwa taarifa ametelekeza mtoto.