Ijumaa , 15th Jul , 2022

Msanii Hussein Machozi amewachana ukweli baadhi ya wasanii wanaofeki maisha kwa sababu ya kulinda brand.

Picha ya msanii Hussein Machozi

"Kwa kazi zetu kwa mfano wanamuziki watu wengi wamekuwa ni wanyonge wa fikra, unyonge wa fikra namaanisha kuwaza mitandaoni mtu atasema nini au raia mitaani wanasema nini bila kujijua nafsi yake anatakiwa afanye nini ajiokoe yeye na famalia yake"

"Mtu anaamua kujifungia ndani asifanye chochote kwa sababu hana gari, hana kitu lakini anataka a-force aonekane ana pesa mwisho wa siku akiwa na kiwanja cha urithi anakauza ili a-maintain ule ustaa kwa sababu pesa hamna kwenye mziki" amesema Hussein Machozi 

Machozi amezungumza hayo kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio ambayo inaruka kila siku ya J3 mpaka Ijumaa saa 7:00 mchana mpaka 10:00 jioni.