Jumapili , 12th Jun , 2022

Rais wa Kondegang, Harmonize ametangaza kushiriki mechi ya hisani ya SAMAKIBA inayokutanisha timu ya nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta na mwanamziki Alikiba kwa ajili ya kukusanya fedha za kusaidia watu wenye uhitaji katika jamii.

Harmonize ameweka wazi atakua timu ya Samatta kupitia ukurasa wake wa instagram, na amejigamba atampoteza Alikiba uwanjani. Mechi hiyo itachezwa uwanja wa Mkapa Juni 18 mwaka huu.