Jumamosi , 5th Nov , 2022

CEO wa Kondegang Harmonize ameweka wazi taarifa ya kuachana rasmi na msanii wake Anjella akieleza kuwa kama kuna anayeweza kuendeleza kipaji chake asisite kujitokeza. 

Picha ya Harmonize na Anjella

Harmonize ameshea ujumbe huo kwenye Insta Story yake unaoeleza kuwa 

"Nilikutana na Anjella akiwa amejikatia tamaa akiwa na ndoto kichwani, sikujiangalia nina kiasi gani niliamini kuwa wapo wanaonisapoti bila kuwalipa senti 5 basi watasapoti kipaji cha sister Anjella".

"Nilichoangalia ni ndoto hasa za mtoto wa kike nimejitahidi kadri ya uwezo wangu najua kuna wenye uwezo mkubwa kunizidi ukizingangatia nimeanza juzi"

"Kama kuna anayeweza kumuendeleza kipaji chake ni faraja kwangu asisite kujitokeza. Puuzia siasa za kusema sijui namdai mahela sikumuuliza kuhusu pesa hata senti 1"