Jumatatu , 28th Mar , 2022

Konde Boy Jeshi Harmonize amefunguka kuwa hakuna video ya ngoma ya mtaje kama ambavyo inadaiwa kutokana na kuonekana kwenye bango la picha yake na Kajala ikiwa ni promo ya video hiyo.

Picha ya Harmonize

Kwenye Insta Story yake Harmonize ameandika kwamba "Hakuna video ya mtaje, narudia tena haya ni mambo binafsi, acha kupost kama unafikiri ni promotions, unaniua".

Harmonize ame-make headlines mitandaoni kupitia maelezo yake kwenye Insta Story akieleza kwamba hana furaha, kuna mtu ame-miss, pamoja na mausala ya kifamilia.