Jumapili , 8th Aug , 2021

Msanii Damian Soul ametamba kusema hakuna ngoma kali ya Amapiano kama mapopo aliyoifanya yeye tofauti na walizofanya wasanii wengine kama Marioo 'mama amina' Diamond Platnumz 'iyo' na Harmonize mang'dakiwe remix.

Msanii Damian Soul

Kupitia EATV & EA Radio Digital Damian Soul ameeleza kuwa "Kusema ukweli hakuna ngoma kama mapopo, siongei kwa sababu ya kujivunia au kujisifu japo kumekuwa na wabishi na wanaokataa, utunzi uliotumika mule sio wa akili ya kawaida"

"Tayari watu kama  Master J, One Credible, Joh Makini, Fid Q  na P Funk Majani wameshaongea kuhusu uwezo na kipaji changu" ameongeza