Jumatano , 20th Mei , 2015

Katika kurejesha muamko wa wasanii hapa Bongo kufanya albam, msanii wa muziki Grace Matata amesema baada ya project yake na Maua Sama, wawili hao wapo katika mpango wa kufanya albam ambayo wataiachia rasmi mwisho wa mwaka.

mwanamuziki wa miondoko ya soul na rnb nchini Grace Matata

Grace ameweka wazi pia juu ya ujio wa kolabo yake akishirikiana na Mwasiti mwanzoni mwa mwezi ujao, rekodi hiyo ikifuatiwa na mufululizo wa rekodi kadhaa kutoka albam hiyo mpya, kabla ya kuiachia yote mwisho wa mwaka.