Gigy Money ameeleza hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya kupost video fupi kupitia 'Insta Live' ya mtandao wa kijamii wa Instagram, akionekana akiwaponda watu wanaoshadadia tukio hilo la kuvuja kwa picha na video hizo.
"Kama nisingekuwa mimi hakuna staa yeyote angeongelea suala la Menina, mbona hawakuongea za Amber Rutty au Nandy hata msamaha aliomba, hakuna mtu anayeweza kupost vile kwa sababu anatafuta kiki, wasipende kumshambulia mtu maana hii mitandao inaweza ikampa mtu msongo wa mawazo au kumpotezea mtu maisha" amesema Gigy Money.
Aidha Gigy ameongeza kuwa, "Hii ni kweli naongea hapa mbele ya kamera nilishawahi kuwaona Mwijaku na Menina Tanga, wakiwa katika gari hata zile video na picha zimevujishwa sidhani kama ni yeye, hawezi kufanya kitu kama kile, hata kutoka kwao kazi maana kuna dini sana, ameacha muziki kwa ajili ya familia yake".
Gigy Money ameendelea kusema, hata alivyosikia Mwijaku amevujisha zile video, alijisikia vibaya kwa sababu aliwaona wakiwa katika mahaba mazito na kama watu wanasema Mwijaku amesambaza video basi ni kweli.