Jumatatu , 11th Aug , 2014

Wanafunzi wa shule za msingi wapatao 700 huko Lindi na Nachingwea wanatarajia kufaidika na msaada wa vifaa vya shule kutoka taasisi ya Flaviana Matata Foundation Stationery Kits.

mwanamitindo Flaviana Matata wa nchini Tanzania

Akiongea katika mahojiano na eNewz mwanamitindo Flaviana Matata amesema kuwa, mpango huu ni kwa ajili ya kuchangia kupunguza changamoto ya vifaa na pia kuboresha mazingira ya kujifunzia wanafunzi kwa kuwapatia vifaa.

Huu ni muendelezo wa mpango wa mwanamitindo huyu wa Kimataifa kuendelea kusaidia wanafunzi hapa Tanzania ambapo tayari kwa kupitia mpango huu amekwishafanikiwa kuzifikia shule kadhaa zilizopo Jijini Dar es Salaam.