Alhamisi , 8th Jan , 2015

Staa wa michano anayebeba heshima kubwa katika gemu ya Hip Hop Bongo, rapa Fid Q amewaeleza mashabiki wake kuwa katika siku za mbeleni hajioni katika mpango wa kuacha muziki, iwe kwa msukumo wa aina yoyote wa mfumo ama maslahi.

Msanii wa Hip Hop nchini Tazania Fid Q

Fid Q amesema kuwa, amepitia ngazi mbalimbali katika muziki, kuanzia yeye binafsi na pia kundi lake kulipa kingilio mlangoni kuingia katika ukumbi kufanya onesho, mpaka ngazi ya kulipwa ili kufanya show, kuonesha kuwa muziki kwake unakuja kabla ya maslahi.

Rapa huyu mkali amesema kuwa, kwa yeyote yule anayekata tamaa kutokana na changamoto za muziki, ni ishara kuwa sanaa hii haipo ndani yake na haimudu, kauli ambayo inawahakikishia mashabiki wa Hip Hop kuwa na rapa huyu kwa miaka mingi zaidi mbeleni ndani ya gemu.