Jumapili , 18th Oct , 2015

Akiwa ni mmoja wa marapa chipukizi wa kike nchini Kenya msanii Shiko Femi One baada ya kufanya vyema na track yake 'Wanjiku Kimani' hivi sasa ameamua kuungana na nyota Chiwawa katika wimbo wao mpya wa pamoja uliobatizwa jina 'Resist'.

msanii wa muziki chipukizi wa nchini Kenya Shiko Femi One

Shiko ambaye ni chipukizi aliyeweza kukubalika sana haswa katika wimbo wa 'Ligi soo' remix alioshirikishwa na mkali Rabbit,hivi sasa amejipanga kutoa kazi na wasanii mbalimbali nchini Kenya ili kuendelea kukuza kipaji chake Afrika Mashariki.

Hivi sasa shiko ameendelea kukuza jina baada ya kufanya trak na Chiwawa ukiwa ni wimbo ambao hivi sasa unatarajia kumpa kumtenegenezea jina katika gemu ya muziki nchini Kenya.