Alhamisi , 8th Jan , 2015

Meneja wa kundi la Mkubwa na Wanawe na TMK Wanaume Family Said Fella amesema kuwa licha ya changamoto kubwa ya mauzo ya albam katika soko la muziki hapa Bongo, atapambana kuhakikisha analirudisha soko hili.

meneja wa Mkubwa na Wanawe, TMK Wanaume Family, Said Fella

Fella ambaye kwa sasa anajipanga kwa ajili ya kutoka na albam ya Yamoto Band, amesema kuwa atatumia uzoefu wake, ubunifu na wadau mbalimbali ili pia kurejesha heshima ya wasanii, waweze kukaa katika ngazi nzuri zaidi wakiwa na mzigo wa Albam.

Mkubwa Fella pia amesema na mashabiki juu ya ujio wa projekti ya wasanii Temba na Chegge ambayo ilifanyika mwishoni mwa mwaka jana huko Afrika Kusini, ikiwa tayari kabisa kutoka Jumamosi hii.