Jumanne , 1st Dec , 2015

Ikiwa ni miaka miwili imetimia tangu kutokea kwa kifo cha muigizaji wa filamu toka Hollywood Paul Walker, waigizaji mwenzake wamemkumbuka kwa kuandika yale wanayohisi mioyoni mwao kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Vin Diesel ambaye waliigiza wote na marehemu Paul Walker kwenye movie ya Fast and Furious 1-7, na kumchukulia kama ndugu kama ambavyo wenyewe wanajiita "Fast & Fusious Family" na umauti kumkuta wakiwa kwenye matengenezo ya filamu yao ya Fast and Furious 7, ameandika "haijalishi uko kwenye ulimwengu gani, utabaki kuwa kaka yangu".

Muigiza huyo ambaye amezidi kujipatia umaarufu baada ya kuachia filamu yake ya The Last Witch Hunter, mwezi august mwaka huu alipokea tuzo ya Teen Choise na kuitoa heshima kwa Paul walker huku akisema katika baraka moja ya maisha yao ni kuwa na fursa ya kumuita Paul kaka.

Nae Tyrese Gibson ambaye ni mmoja wa wanafamilia ya Fast & Furious, mara kwa mara amekuwa akimkumbuka Paul Walker kwa kupost vitu mbali mbali kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, leo amewataka watu wazidi kumuombea Paul Walker huku akisema ni ngumu kwake.

Paul Walker anatimiza miaka miwili tangu afariki dunia kwenye ajali ya gari, huku familia yake ikiwa imefungua kesi wakiituhumu kampuni ya magari aina ya Porsche kuwa inahusika kwa kifo cha Paul.