Emmanuel Mbasha
Mbasha mwenye umri wa miaka 32 ambaye ni mume wa Mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha, Juni 16 alifikishwa Mbele ya Hakimu Hakimu Mkazi Wilberforce Luago na kusomewa mashtaka mawili ya ubakaji.
Wakili wa Serikali Nassoro Katuga alidai kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo mawili maeneo ya Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam, ambapo shtaka la kwanza alitenda kosa hilo Mei 23 mwaka huu Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, Jijini Dar es Salaam alimwingilia kwa nguvu shemeji yake wa kike.
Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Mei 25, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria, mshtakiwa aliumuingilia kwa nguvu mfanyakazi wake. Hata hivyo, Mbaha alikana mashitaka hayo .
Kesi hiyo ya Mbasha imehairishwa hadi Julai 17, mwaka huu ambapo itatajwa tena kwa ajili ya mtuhumiwa kusomewa maelezo ya awali kabla ya kuanza kusikilizwa rasmi kwa kesi inayomkabili.