Jumatano , 4th Mar , 2015

Staa wa muziki kutoka Sudan, Emmanuel Jal anatarajia kushiriki katika mjadala mkubwa kuhusiana na uhusika wa wanaume katika mapambano ya kupigania usawa wa kijinsia huko London.

msanii wa muziki wa nchini Sudan Emmanuel jal

Mjadala huo unatarajiwa kufanyika Jumatatu Machi 9, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Katika mjadala huo ambao utarushwa katika vyombo vya habari, Emmanuel Jal atashiriki pamoja na mwigizaji maarufu, Meghan Markle ambao wataelezea uzoefu wao katika mada hiyo kutokana na mazingira waliokulia.

Emmanuel Jal ambaye katika utoto wake alikuwa mwanajeshi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Sudan, amekuwa akishirki katika harakati mbali mbali za kupigania amani haki na usawa katika jamii, hii ikiwa ni nafasi nyingine ya kipekee kwake kutekeleza jukumu hilo.