Alhamisi , 20th Feb , 2014

Rapa wa kimataifa kutoka Marekani, Eminem anatarajia kutua huko Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya onyesho kubwa kabisa ndani ya Jiji la Cape Town katika ziara iliyopatiwa jina The Rapture 2014.

Onyesho ya Eminem litafanyika ndani ya uwanja wa Ellis Park tarehe 26 mwezi huu na litakuwa ni maalum pia kwa ajili ya rapa huyu kutangaza albam yake mpya inayokwenda kwa jina “The Marshall Mathers LP 2”.

Msanii huyu pia atafanya onyesho lingine huko Johannesburg pia kabla ya kumaliza ziara hii kubwa ambayo ni ya kwanza katika historia ya msanii huyu katika majiji haya makubwa Kusini mwa Afrika.