Ijumaa , 14th Oct , 2016

Msanii King Crazy Gk ameishukuru EATV LTD kwa kuanzisha EATV AWARDS, kwani licha ya kuinua sanaa lakini pia itatekeleza sera ya Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki, upande wa sanaa.

GK

Akizungumza na EATV King Crazy Gk amesema EATV AWARDS ni kitu kikubwa na yeye kama msanii anaisubiri kwa hamu, kuona ni jinsi gani itasaidia kuwaunganisha wasanii wa Afrika Mashariki.

“Ni kitu kikubwa ambacho mi nakiogopa, kwa sababu hii ni tuzo ya kwanza katika East Afrika, ile East Africa Comunity ndiyo ina'make' sense, ndiyo mnaitengeneza katika muziki, big up kwa East Africa kwa kuweza kutambua mchango wa artist wa East Africa kutuleta pamoja, tunaisubiria kwa hamu”, alisema King Crazy GK.

Pia Crazy Gk aliendelea kusema kwamba ana imani EATV AWARDS zitafika mbali kwani imeanzishwa na watu ambao wanajua nini wanafanya.

“East Africa ilipokujaga watu walikuwa wanaona kama kichekesho, lakini baada kama ya miaka miwili naenda Kenya, Uganda nakuta mpaka chooni kwenye mahoteli nakuta East Afrca Tv, kwa hiyo East Africa wanapoanzisha kitu, nina hakika kitaenda mbali na kitafanya vizuri”, alisema Crazy GK.

Tags: