Alhamisi , 22nd Sep , 2016

Msanii Ruby ambaye leo ameachia wimbo wake mpya wa 'wale wale', amezizungumzia EATV AWARDS na kusema zitaongeza changamoto kwa wasanii.

Ruby ndani ya EA Radio

Akizungumza na East Africa Radio, Ruby amesema tuzo hizo kuanzishwa na kituo cha habari anaamini zitakuwa na hamasa kubwa kwa wasanii, kwani ni kama zawadi kwao.

"Nimezipokea kwa heshima kubwa sana kwa sababu tuzo ni kitu kikubwa sana, ni zawadi naiheshimu sana, naona kabisa italeta changamoto, kwa sababu ni media pia imekuja na awards zake, itaongeza ushindani mkubwa sana kati ya watu katika kupata kitu ambacho kinaonesha kwamba umefanya kazi nzuri, itasaidia kuongeza chachu ya ufanyaji kazi sana", alisema Ruby.

EATV AWARDS zinatarajia kufikia kilele chake tarehe 10 Desemba 2016, na zitahusisha wasanii wa muziki na filamu wa nchi za Afrika Mashariki, kwa udhamini mkubwa wa Vodacom Tanzania.

Tags: