Jumanne , 21st Apr , 2015

Msanii Dully Sykes kwa kutumia busara zake ameongezea uzito kuwashauri vijana kutumia nafasi ya kujiandikisha ili kuweza kupiga kura mwaka huu, licha ya changamoto ya taratibu na foleni katika mazoezi kama haya.

msanii wa bongofleva Prince Dully Sykes

Dully Sykes, ameongea na vijana wenzake akiwa kama staa mwingine mkubwa wa muziki Bongo kuunga mkono kampeni ya Zamu Yako 2015, kutaka kundi hilo kubwa lenye uwezo mkubwa katika jamii kutumia nafasi yao vizuri mwaka huu.