Jumamosi , 25th Apr , 2015

Staa wa muziki Dully Sykes ambaye kwa sasa anajipanga kwa ujio mkubwa kabisa kuanzia wiki ijayo, ameweka wazi kuwa, video ya kazi hiyo ameitayarisha kwa Director Adam Juma ambaye amekuwa na historia ya kufanya naye kazi kwa miaka mingi sasa.

Dully Sykes

Licha ya mabadiliko yanayoonekana sasa katika soko la videos za muziki, Dully ambaye ni mkongwe katika game ya Bongo Flava, ameeleza kuwa bado imani yake kubwa ipo kwa Adam Juma, akiwa na matumaini ya kuendelea kufanya naye kazi kwa imani kuwa atafika mbali zaidi.