Msanii Dully Sykes
Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Dully Sykes amesema yeye ana wivu sana, hivyo akiwa kwenye mahusiano na mwanamke ambaye anapenda umaarufu wa kwenye kamera hataweza kuhimili mikiki yake.
“Sijawahi kupenda mwanamke anayependa kamera, naona shida za mastaa na mademu , naona yanayowatakea wadogo zangu, mimi Mungu ameniumba na wivu sana, vile vitu siwezi kuvumilia”, alisema Dully Sykes.
Dully Sykes aliendelea kusema kuwa kama aliwahi kuwa na mahusiano na mtu maarufu basi haikuwa ‘serious’, lakini yeye hupenda wanawake ambao hawana umaarufu.