Jumatatu , 4th Mei , 2015

Msanii mkongwe katika gemu ya Bongo Flava, Dudu Baya ambaye kwa sasa amekuwa na ukaribu mkubwa na aliyekuwa hasimu wake mkubwa, Mr Nice akiweka nia yake ya kufanya naye kazi ya pamoja.

Wasanii wa bongofleva nchini Dudu Baya na Mr Nice

Dudu amesema kuwa mpaka sasa kinachochelewesha kolabo kati yao, ni mtindo wa muziki wa TAKEU ambao Nice anaufanya.

Dudu amesema anaweza kuingia studio kufanya ngoma na Nice endapo atabadilika na kufanya rekodi yenye mahadhi mengine kutokana na msimamo alionao kuwa hawezi kunengua hata siku moja.

Vilevile Dudu Baya akatumia nafasi hiyo kulaumu wasanii wanaofanya Bongo Flava kukosa ubunifu, akiweka wazi kuwakubali wasanii kama Yamoto Band ambao kwa sasa wanafanya vizuri.