Dudu Baya alia na kufungiwa kwa viroba

Sunday , 13th Aug , 2017

Msanii Godfrey Tumaini maarufu kama Dudu Baya, amesema kitendo cha serikali kufungia pombe aina ya viroba kumemuathiri kwa kiasi kikubwa, kwani na yeye alikuwa mtumiaji wa kilevi hiko.

Msanii Dudu Baya

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Dudu Baya amesema alikuwa anakunywa viroba kama pombe ya kawaida kwani ina ubora ule ule na ya kwenye chupa.

"Unajua mi sivuti sigara, situmii unga, kilevi ninachotumia ni bapa, hata nikiwa na mke wangu nampa hela akanunue bia mi nanunua bapa yangu napiga, lakini mara nyingi nikiwa mtaani naagiza viroba vyangu nakunywa, unajua hii ni sehemu na ile ambayo ipo kwenye chupa, haina tofauti, kwa nini nione kinyaa kutumia viroba, mi sina ubishoo, kwa hiyo kidogo kufungiwa kwa viroba kumenimuiza", alisema Dudu Baya.

Mnamo mwezi Februari mwaka huu serikali ilipiga marufuku uzalishaji na utumiaji wa pombe aina za viroba, ambayo inaelezwa kuathiri vijana wengi na kuzorotesha uzalishaji mali kwa uchumi.