Jumamosi , 5th Sep , 2015

Wasanii wa kundi kongwe la muziki la la Dru Hill na Jagged Edge kutoka Marekani, wanatarajiwa kuitikisa Afrika Mashariki ambapo watatua Kenya mwezi Oktoba kwa ajili ya onesho kubwa na la mara ya kwanza kabisa katika eneo hili la Afrika.

Dru Hill

Katika tukio kubwa kabisa la kiburudani ambalo limepatiwa jina triple-treat affair, kundi la 112 pia litakuwa miongoni mwa watumbuizaji, lengo likiwa ni burudani na pia kukumbuka burudani za miaka ya nyuma wakati makundi haya yanatawala chati za muziki.

Ujio wa nyota hawa wakubwa, unatarajiwa kuwafuta machungu wapenda burudani wengi ambao waliguswa na kuahirishwa kwa ujio wa kundi hilo la Jagged Edge nchini Kenya mwaka 2009, baada ya makubaliano kati yao na mratibu wa show kutokufikia muafaka.