Alhamisi , 16th Nov , 2023

Drake ameachia video ya ngoma yake inayofahamika kama''First Person Shooter'' kwenye ngoma hiyo ambayo Drake kamshirikisha J cole, 

Drake & J cole

 

kuanzia dakika 1 sekunde ya 39 kinaonekana kipande ambacho madhari iliyotengenezwa inafanana na ile ya picha ya Messi na Cristiano Ronaldo wakati wanafanya tangazo la chapa maarufu nchini Ufaransa. (Jina kapuni)

Picha ya Messi na Ronaldo, iliwekwa mitandaoni mwaka 2022, ikiwaonyesha wakicheza mchezo maarufu unaofahamika kama ''chess'' picha hiyo ilitembea sana mtandaoni kutokana na ubora wa wachezaji hao na namna ambavyo watu wengi wamekuwa wakilinganisha ubora wao.

Hapa kwenye wimbo wa Drake kulingana na picha ile, Drake ndiye aliyekaa upande wa Messi na J cole akachukua upande wa Ronaldo.

Yote ni kuhusu ubunifu, Cole na Drake wamefanikiwa au waliishiwa ubunifu?

Picha: Annie Leibovitz