Jumanne , 10th Nov , 2015

Msanii a muziki Dr John kutoka kundi la Wagosi wa Kaya, ameamua kutoa msaada kwa wasanii wengine wanaotoka Tanga, katika harakati za kunyanyua mkoa huo kisanaa baada ya mchango na nafasi yake kubwa katika gemu ya Bongofleva.

Dr. John na Fredy Mkoloni

Dr John ameeleza kuwa mpango huo anautekeleza kupitia kundi alilotengeneza la Hip Hop ambalo linatambulika kwa jina The Family, baada ya kuona kuna vipaji vingi kwa upande wa sanaa hiyo katika mkoa wake, ambavyo havijapata msaada wa kuzielekea ndoto zao.

Kuhusiana na hili, Dr. John anaeleza zaidi mwenyewe hapa.