Jumapili , 22nd Feb , 2015

Mbunifu wa Mitindo ya mavazi mwenye rekodi ya kushida tuzo za kimataifa, Doreen Mashika kutoka Zanzibar, amejipanga kudhihirisha kwamba kanuni za msingi katika tamaduni jadi barani Afrika bado zina nguvu katika mitindo.

Doreen Mashika

Doreen atadhihirishahayo kupitia Onesho la mavazi lijulikanalo kama ‘Fashion Night In by Doreen Mashika’ litakalofanyika jijini Dar mwishoni mwa mwezi huu.

Onesho hilo litahusisha wanamitindo mbalimbali kutoka Kenya na Tanzania na pia litahusisha muandaaji kutoka nchini Uingereza, kwa upande wake akijikita zaidi katika kugundua bidhaa ambazo zitakidhi haja za waafrika, zikileta pamoja uasili na usasa zaidi.

Kupitia onesho hilo, Doreen anatarajia kuonesha ni kwa namna gani mwanamitindo anavyoweza kuonekana wa kisasa katika njia zaidi za asili na za jadi.