
Dorah ametoa kauli hiyo, wakati akizungumza kwenye kipindi cha Kikaangoni kinachoruka kila siku ya Jumatano kupitia kurasa za Facebook na Youtube za East Africa TV, na kumtaja jina la Edson ambaye kwa sasa bado ni mwanafunzi wa chuo.
"Kwa sasa mpenzi wangu anamiaka 23 na mimi nina miaka 24 na nilianza naye nilipokuwa nimemaliza kidato cha nne, kifupi huyu ni mpenzi wangu wa kwanza, na mtu akisema nambemenda atakuwa ameamua yeye tu kusema" amesema Dorah.
Aidha Dirah ameongeza kuwa,"kingine kwa sasa anasoma Iringa, mwingine akisema mimi natoka na Kibenten bado simkatazi, kwa sababu atakuwa ameamua yeye"
Tazama mahojiano kamili