
Demarco
Demarco ambaye amekwishafanya kazi yenye mafanikio na msanii Peter Miles, atatumbuiza katika tamasha la Street Jam, akiwa na sapoti kutoka kwa wasanii Chameleone, Mun G, Vampino na wengine ambapo kutoka orodha hii, wasanii hawa wapo katika nafasi kubwa kuwepo katika orodha ya kolabo alizopanga kufanya staa huyu wa kimataifa.
Ujio wa Demarco Afrika Mashariki, unafuata ujio mwingine mkubwa wa staa kutoka Jamaica, Konshens ambaye sasa yupo huko Kenya kwaajili ya onyesho kubwa la muziki litakalofanyika hapo Kesho.