Jumatano , 29th Jun , 2016

Rapper Dogo Janja ambaye kwa sasa anazidi kupasua mawingu kwa ngoma yake ya 'My life remix', amekiri kuwa kuna stari kwenye wimbo huo kuna mstari alimuimba Young Dee kuhusu kutumia madawa ya kulevya.

Mstari huo unaosikika ukisema "mtaongea sana nyie ma-young hamniwezi, mtazidi kupenga kisa stress mpaka totoro, nawanyima chakula mwaka huu mule magodoro", Dogo Janja akiongea kwenye eNews amesema lilikuwa ni kama jiwe gizani lakini anashukuru lilimfikia muhiska na hatimaye amejitokeza na kukiri kutumia madawa ya kulevya.

"Limeweza kuwa jiwe gizani, limemlenga muhusika kajionyesha na kukubali kutumia na kaacha, tumuombee Mungu aende mbele asirudi", alisema Dogo Janja.

Mwandishi wa eNews alipomuuliza kama muhusika ni Young Dee, Dogo Janja alikiri kuwa ndiye muhusika aliyemlenga kwenye mstari huo, na kwamba ndio muziki wa hip hop ulivyo, na kutupiana madongo.

Young Dee