
Kushoto ni Alikiba, kulia ni Dj Seven
Dj Seven amesema haoni tofauti kufanya kazi na msanii mwingine nje ya Konde Gang kwa sababu mziki ni biashara na yeye anatafuta kitu kitakacholeta faida.
"Kuna msanii ambaye anamiliki lebo nimemuomba kufanya naye kazi kama itakuwa poa tutafanya, nataka kufanya kazi na Alikiba tumeshaongea na Producer wake Yogo kila kitu kikiwa sawa tutafanya wimbo" ameeleza Dj Seven Worldwide
Mpaka sasa Dj huyo ameshafanya kazi na wasanii mbalimbali wa BongoFlava kama Young Lunya, Salmin Swaggz, Linah, Mimi Mars na Baddest.