Dj Madtraxx wa nchini Kenya
DJ huyo ametoa kauli hiyo hivi karibuni wakati wadau na baadhi ya wasanii wa muziki wakiwaelekezea lawama zaidi Madjs kwa kutopiga zaidi nyimbo za ndani na kuelekeza nguvu zaidi kwa wasanii wa nje.
DJ Madtraxx ametoa ya moyoni akisema kuwa yeye binafsi hatopoteza muda wa kuzicheza nyimbo ambazo hazina viwango vya kukidhi na ataendelea kuzicheza nyimbo zozote ulimwenguni ilimradi tu zikidhi viwango vinavyostahili katika tasnia ya muziki.







