Jumanne , 17th Nov , 2015

Msanii Harmonize amesema video nyingi za wasanii toka East Africa hazifanyi vizuri kutokana na wasanii kuamini director anaweza kuwa na stori nzuri kuliko msanii, jambo ambalo sio kweli

Harmonize ameyasema hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kueleza kuwa msanii ndiye aliye na stori nzuri ya wimbo wake, hasa kwa directors wa nje kwani hawajui muziki wa East Africa unataka nini.

“ Video nyingi za East Africa tunakosa kuzifanya vizuri kwa sababu tunaamini director anaweza akawa na story nzuri kuliko msanii ambaye ameandika wimbo, lakini ukweli ni kwamba wewe ambaye umeandika wimbo unaweza ukawa na story nzuri sana ya video kuliko hata director, hasa director wa nje hawajui muziki wetu wa East Africa unataka nini”, alisema Harmonize.

Pamoja na hayo msanii huyo chipukizi anayekuja kwa kasi kwenye muziki wa Bongo Flava, amewataka wasanii kuwa wabunifu wa stori zao wenyewe na kuwakabidhi watengenezaji wa video huku akiwaachia kwa ushauri na kusimamia.

“Mi nashauri kwa wasanii wengine ambao wanataka ku 'shoot' na ma director wa nje, create story we mwenyewe, mwambie director nataka kwenye video iwe hivi, alafu director atoe tu kama ushauri ongezea hiki, hiki na hiki, tutakuwa tunafanya video nzuri kila siku”, alisema Harmonize.