Jumatano , 9th Apr , 2014

Msanii wa muziki ambaye nyota yake inang'ara ndani na nje ya mipaka ya Bongo, Ommy Dimpoz leo hii ametumbukia Kikaangoni Live kupitia kipengele cha ukurasa wetu wa facebook, ambapo wapenzi wa muziki na wapenda burudani wameweza kuchat naye live.

Ommy Dimpoz

Ommy Dimpoz ameonyesha mapenzi makubwa aliyonayo kwa mashabiki wake kwa kutumia muda wa saa mbili kujibu moja kwa moja maswali kibao ambayo mashabiki wake 'wamemkaanga' nayo.

eNewz baada ya kufuatilia zoezi zima kwa karibu tukakutana na Ommy Dimpoz na kumpima joto la Kikaango, ambapo msanii huyu amesema kuwa, amefurahia nafasi hii hasa ikizingatiwa kuwa ukurasa wake binafsi wa facebook uliingiliwa na kuibiwa na wezi wa kimtandao na hivyo kumkosesha nafasi ya kuwasiliana na mashabiki wake kwa njia hiyo.

Endelea kuwa sehemu ya familia kubwa ya wapenzi wa ukurasa wa facebook wa EATV, shiriki ukurasa huu na marafiki na Like pia kama bado hujafanya hivyo na kumbuka, Wiki ijayo tunakuletea staa mwingine mkali ambaye utachat naye moja kwa moja.

kufuatilia maongezi ya Dimpoz na mashabiki wake Kikaangoni, fuata link hii https://www.facebook.com/eatv.tv/photos/a.159892260691867.39844.15730328...